Jomvu: Serikali iingilie maswala ya ardhi

Msemaji wa Jamii ya Wajomvu Ahmed Kombo Ahmed amewataka viongozi wa serikali kuingilia kati na kusuluhisha mzozo wa ardhi ambayo wakaazi wanapuuza agizo la mahakama.

Hii ni baaada ya baadhi ya wanaopima ardhi ya eneo la jomvu kupuuza maagizo ya mahakama kutokana na mvutano wa ardhi katika eneo hilo akiwalaumu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa kina mama,watoto na vijana.

Aidha, amewaomba wajomvu wawe watulivu na kuiomba taasis ya haki za binadam na serikali kwa jumla kuingilia kati baada ya maafisa wa polisi kuwa fyetulia risasi na vitoa machozi wakati wa maandamano siku chache zilizopita.

Amesema hawatarudi nyuma hadi haki itendeke.

Haya yanajiri baada ya wakaazi wa Jomvu kuu kuandamana siku ya juma tatu wakilalamikia kunyang’anywa kipande chao cha ardhi ambayo wamekuwa wakiishi zaidi ya karne nane.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi