Na siku moja tu baada ya mkataba wa muungano wa Kenya kwanza kuhusu jinsi watakavyo gawa vyeo endapo wataunda serikali mwezi wa nane kuwekwa wazi hisia mseto zinazidi kutolewa.
Wa hivi punde ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed.
Akiongea kwa niaba ya muungano wa Azimio la umoja one Kenya mjini Malindi Junet amemsuta naibu rais Dkt. William Ruto akimtaja kiongozi ambaye anajitakia makuu na wakenya wanafaa kuwa makini kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa kuepuka viongozi wanao jail maslahi yao binafsi.
Katika mkataba huo wa Kenya kwanza unapendekeza cheo cha waziri mkuu kwa kinara wa chama cha ANC, cheo cha uspika wa bunge la kitaifa kwa kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula na uspika wa bunge la seneti kwa gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi.