Jurgen Klopp Achaguliwa Kama Mkufunzi Bora Wa Ligi Ya EPL

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amechaguliwa kuwa meneja bora wa msimu wa EPL na kushinda taji la Sir Alex Ferguson kama meneja bora wa mwaka wa LMA.

Liverpool walichukua nafasi ya pili kwenye mbio za ubingwa, wa ligi ya primia wakijikusanyia alama 92.

Also Read
Shule Ya Kitaifa Ya Kenyatta Yaibuka Bora Taita Taveta

Akitafakari kuhusu kutamatika kwa msimu wa Ligi kuu wakati akipokea tuzo yake, Klopp alisema: “Ni heshima kubwa na ulikuwa msimu wa kichaa. Siku ya mwisho ya mechi ambapo michezo miwili pekee haikuwa na maana na, katika iliyobaki, sote tulicheza kwa ukamilifu. kila kitu.

“Ilikuwa hali ya wasiwasi kidogo, haikuwa matokeo bora kwetu, lakini tayari tumeimaliza. Na unaposhinda tuzo kama hii wewe ni gwiji, au una timu bora zaidi ya ukocha duniani niko hapa na wanne wa wakufunzi wangu, na wanajua jinsi ninavyowathamini.”

Jurgen Klopp ameiongoza Liverpool kutwaa Kombe la FA na Kombe la Carabao msimu huu Liverpool wanaweza kutwaa kombe la tatu ikiwa wataifunga Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi mjini Paris

  

Latest posts

Ofisi Ya Msajili Yawashirikisha Washikadau Kwenye Msafara Wa Amani Pwani

Ruth Masita

Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Viwango Vya Elimu Jomvu

Ruth Masita

WRC Safari Rally Kuandaliwa Naivasha

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi