Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, amesema aliamua kuhudhuria mahojiano ya kutafuta mgombea mwenza wa kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, ili kuondoa mbali shauku kuhusu kujitolea kwake kwa muungano huo.
Kalonzo alifika mbele ya jopo la uteuzi linalowasaili wawaniaji wa wadhifa huo licha ya kusema awali kuwa hatakubali kufika mbele ya jopo hilo la wanachama saba.
Kalonzo amesema sasa hakuna sababu ya jopo hilo kutomteuwa kuwa mgombea mwenza wa Raila.
Aliyekuwa mbunge wa Gatanga, Peter Kenneth, alikuwa wa pili kusailiwa baada ya Kalonzo.