Kamati Ya Utekelezwaji Wa Miradi Ya serikali Yazuru Bandari Ya Mombasa

Kamati kuu ya kitaifa ya kiufundi na serikali inayosimamia utekelezwaji wa miradi na mipango imetembelea bandari ya Mombasa  kukagua vifaa na utendakazi wake.

Kamati ya ufundi ya kitaifa ya utekelezaji wa maendeleo (NDITC) ikiongozwa na mwenyekiti wake Dkt. Karanja Kibicho imeeleza kuridhishwa na maendeleo ambayo yameifanya bandari hiyo kuwa na ufanisi sawa na ushindani.

Also Read
Vijana Wahimizwa Kujiajiri Kwale

Kibicho ambaye pia ni katibu mkuu wa mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa aliandamana na msafara wa makatibu wakuu na kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari hiyo nchini John Mwangemi.

Also Read
Mfanyakazi Wa Meli Afariki Bandarini Mombasa

Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi unaoendelea wa jengo la pili la makasha katika kituo hicho na ukaguzi wa kituo kipya cha mafuta cha Kipevu.

Also Read
Shughuli Za Bandari Hazijaathirika Asema Mkurugenzi Salim

Bandari ya Mombasa imesalia kuwa katika nafasi ya juu ya 120 bora duniani 6 barani Afrika na imeunganishwa kwa zaidi ya bandari themanini kote duniani.

 

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi