Kamishna wa kaunti ya Kwale awataka wazazi kuripoti mapema visa vya unyanyasaji

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewataka wazazi kuripoti kesi za unyanyasaji wa kingono mapema miongoni mwa watoto ili kukomesha tabia hiyo ya kinyama.

Also Read
Serikali yasimamisha ujenzi wa zahanati kwa shamba ya shule huko Malindi

Kamishna wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amesema ucheweleshaji wa kuwasilisha kesi hizo kumechangia pakubwa changamoto katika kupigania haki za watoto waliodhulumiwa.

Kanyiri amedokeza kwamba wahalifu wengi hutembea huru kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi mwafaka uliopotea kutokana na kukawia kuripoti kesi hizo kwa afisi husika.

Also Read
Walimu kaunti ya Kwale wasisitizwa kuzingatia sheria za covid-19 shuleni

Hata hivyo ametaka jamii kutowaficha wahalifu na kuijulisha idara ya usalama pindi uovu huo unapotendeka.

Also Read
Waakazi wa Jomvu kuu waanza zoezi la kumtimua MCA

Aidha ameapa kuchukua hatua kali dhidi ya washukiwa wa unyama huo.

 

  

Latest posts

Mbelle Awahimiza Vijana Kuzidisha Chachu Ya Talanta Zao

Clavery Khonde

Rais Kenyatta Amekutana Na Rais Biden Wa Marekani

Clavery Khonde

Walioathirika Na Ujenzi Wa Bwawa La Mwache Kufidiwa Kabla Ya Mwezi Disemba

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi