Serikali ya kaunti ya Kilifi iko mbioni kuzindua rasmi wodi ya kuwashughulikia wagonjwa wa maradhi ya saratani ili kuwapunguzia mzigo wanaougua maradhi hayo.
Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm kwa njia ya simu waziri wa afya wa kaunti ya Kilifi Charlse Dadu amesema kwa sasa awamu ya kwanza ya wodi hio katika jumba la Kilifi medical complex iko karibu kukamilika nan i hivi karibuni watazindua rasmi wodi hio.
Aidha ameutaja uhaba wa wahudumu wa afya kama changamoto kubwa katika kaunti hio akisema wle wako hawatoshelezi matakwa ya wakaazi wengi wa kaunti hio na amedokeza kuwa serikali ya kaunti hio iko mbioni kuwaajiri wahudumu wa afya zaidi ili kukidhi mahitaji ya wanahitaji huduma za afya kwenye kaunti ya Kilifi.