Kaunti ya Kilifi yaanza uboreshaji wa huduma za afya

Serikali ya kaunti ya Kilifi imeweka mikakati ya kutosha ili kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza idadi ya wadi za wagonjwa katika hospitali kuu ya mji wa Malindi.

Kulingana na gavana Gedion Mung’aro,hatua hizo zitaanza kutekelezwa kuanzia juma lijalo kupitia ufadhili wa kampuni tofauti ili kutatua changamoto za maswala ya afya.

Also Read
Lalama Za Uteuzi Wa ODM Mombasa

Akizungumza mjini malindi baada ya kufanya ziara katika hosipitali hiyo, Mung’aro amedokeza kuwa serikali yake inalenga kuyaangazia kwa upesi maswala ya afya, kilimo, barabara miongoni mwa mengineyo.

Also Read
Rais William Ruto asema wauzaji wa dawa za kulevya chuma chao kimotoni

Kauli hiyo imeungwa mkono na diwani wa wadi ya Shella mjini humo Twaher Abdhulkarim , huku akidai kuwa serikali ya kaunti hii ina mipango kabambe ya kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Also Read
Shirika la UNICEF laikabili wizara ya elimu barakoa laki saba kwa ufunguzi wa shule

Hata hivyo Twaher amebainisha kuwa juhudi za gavana wa kaunti hii zitafanikiwa kupitia ushirikiano wa viongozi wote.

  

Latest posts

Mvurya Ataka Maafisa Wa Idara Na Mashirika Ya Serikali Kuhusu Maendeleo Zishirikishe Serikali Za Ugatuzi

Ruth Masita

Wanawake Wajasiriamali 450 Wanufaika Na Mafunzo Ya Kibiashara Mombasa

Ruth Masita

Mahakama yamwachilia mbunge wa Sirisia John Walukhe kwa dhamana ya shilingi milioni kumi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi