Kemnac Yakashifu Ushoga Shuleni

Baraza kuu la ushauri kwa waislamu nchini KEMNAC wamelaani vikali msimamo wa waziri wa elimu profesa George Magoha kuhusu msimamo wake kuhusu mashoga shuleni.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza hilo la KEMNAC Sheikh Juma Ngao wamemtaka Magoha kubadilisha msimamo wake ndani ya saa 72 la sivyo wataelekea mahakamani kumshtaki.

Also Read
Wakaazi wa Kilifi Wanufauika na Mradi wa Ugavi wa Chakula

Kadhalika Sheik Ngao amemtaka rais Uhuru Kenyatta aingilie  kati na abuni kitengo maalum ambalo litawapa wanafunzi hao wanaoshiriki ushoga shuleni hamasa lakini si kukubali utovu huo wa nidhamu kuendelea ndani ya jamii.

Also Read
Walimu Wakuu Wameagizwa Kutowarudisha Nyumbani Wanafunzi Kwa Kukosa Karo

Sheikh Amir Zani mkurugenzi wa Madrassa na mwenzake wa elimu katika baraza hilo Hafidh Muhsin pia ni miongoni mwa waliokashifu hatua hiyo ya profesa Magoha na wakamtaka kubadili msimamo wake haraka iwezekanavyo ili kulinda maadili ya jamii.

Also Read
Elungata Awahakikishia Watahiniwa Usalama Wakati Wa Mitihani Pwani

Itakumbukwa kwamba ni hivi majuzi ambapo waziri wa elimu Profesa George Magoha alitaka wanafunzi wanoshiriki ushoga kutokubaliwa ndani ya shule za mabweni lakini wakakubaliwa katika shule za kutwa.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi