Kenya Yapiga Marufuku Safari Za Ndege Kutoka India

Serikali imepiga marufuku usafiri wa Ndege kutoka taifa la India ambako maambukizi ya virusi vya Corona yanazidi kuongezeka  sawia na idadi ya juu ya vifo vinavyoshuhudiwa  katika taifa hilo.
Akiongea mjini Voi kaunti ya Taita Taveta waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema serikali imechukukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wananchi wake huku wale wanaotaka kusafiri kuja hapa nchini wakipewa saa 72 kufanya hivyo.
Kagwe aidha anasema wale wote watakaoingia hapa nchini kutoka taifa la India watalazimika kuwa Katika karantini ya siku 14 huku ndege za mizigo pekee zikiruhusiwa kusafiri hadi taifa hilo.
Kadhalika Kagwe amesema watu 198 wako katika chumba cha wagonjwa mahututi na kusema kwamba serikali itaanza kuagiza dozi za chanjo aina ya Johnson and Johnson na ile ya Pfizer Katika majuma mawili yajayo.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi