Kenya Yarekodi Idadi ya Juu ya Vifo Vinavyotokana na Covid-19 Kote Afrika.

Kituo cha Afrika cha kukabiliana na maradhi kimesema kwamba Kenya imenakili ongezeko la asilimia 33 ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19 katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Uchunguzi wa kituo hicho uliofanywa kwa ushirikiano na muungano wa Afrika katika muda wa majuma manne yaliopita, ulibaini kuwa kenya ilirekodi vifo zaidi vilivyotokana na Covid-19 kuliko mataifa mengine ya kiafrika kulingana na idadi yake ya watu.

Also Read
Uhaba Wa Chanjo Ya AstraZeneca

Kenya ilifuatiwa na Afrika Kusini ambayo ilinakili asili mia 30 ya vifo hivyo huku Jamhuri ya Congo ikiwa ya tatu na ongezeko la asili mia tisa.

Also Read
Idara Ya Misitu Ya Waonya Wakaazi Wa Kwale

Kulingana na kituo hicho cha CDC, kumekuwa na ongezeko la jumla la asili mia 21 ya vifo vipya vya ugonjwa wa Covid-19 vinavyonakiliwa barani Afrika kila wiki.

Also Read
Serikali Imetakiwa Kuwahamasisha Wakenya Kuhusu Chanjo Ya Korona

Kituo hicho kiliongeza kwamba Kenya ilikuwa ya tatu barani afrika baada ya kunakili ongezeko la asili mia nne la maambukizi ya virusi vya Corona.

  

Latest posts

Kinara wa ODM Raila Odinga awahimiza wadau wa sekta za kiuchumi kubuni zaidi fursa za kustawisha uchumi

Joshua Chome

Naibu rais alilaumu bunge kwa kuchelewesha utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote

Joshua Chome

Tume ya uchaguzi yaagizwa kufika bungeni kuelezea maandalizi ya uchaguzi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi