Wakaazi wa Chakama eneo bunge la Magarini wanaendelea kulalamikia uvamizi wa ndovu ambao wanasema wanamaliza mimea yao waliyokua wakitarajia kuvuna.
Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm wakaazi hao wakiongozwa na Mwambegu Kiponda wanasema mazao yao waliotarajia kuwa yangewanufaisha yanavamiwa na ndovu kila kukicha huku wakisema mazao ya tikitii maji ndio yameathirika zaidi kutokana na vuliwa na hayawani huyo.
Aidha wameshangazwa na kitendo cha viongozi wa eneo hilo cha kutoingilia kati swala hilo ili waweze kuhakikisha wanawashinikisha maafisa wa shirika la uhifadhi wa wanyamapori KWS kuwadhibiti ndovu hao.