Kinara wa chama cha PAA aliye pia gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jeffa Kingi ameuhama rasmi muungano wa Azimio la umoja wa one Kenya na kujiunga na muungano wa Kenya Kwanza unaongozwa ni Naibu wa Raisi William Ruto.
Akiongea katika makaazi rasmi ya naibu wa raisi jijini Nairobi Kingi amesema PAA imechukua uamuzi huo baada ya muungano wa Azimio kudinda kuweka sahihi ya kuyashughulikia mapendekezo yao makuu.
Kingi akisema mkataba wa makubaliano ndani ya muungano wa Azimio la umoja wa One Kenya umekuwa wa siri kubwa kwa viongozi wachache.
Gavana Kingi wameweka makubaliano manane ambayo yaliwekwa sahihi kisheria na yatatekelezwa endapo muungano wa Kenya kwanza utashinda.
Ni kauli iliyoungwa mkono na naibu rais dkt. William Ruto akisema matakwa ya wakaazi wa pwani yatatiliwa maanani ndani ya muungano wa Kenya kwanza.