Kitendawili Cha Ardhi Taita Taveta

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta kupitia idara ya ardhi imesema kuwa, haitakubali kuendelea kusuluhisha mizozo ya ardhi inayosababishwa na wadau wengine bila kuhusisha idara hiyo kuanzia mwanzo wa chimbuko la mizozo hiyo.
katibu wa ardhi kaunti ya Taita Taveta Mwandawiro Mghanga amepinga madai kuwa serikali ya kaunti hiyo imehusika katika zoezi la kuwafurusha Wakaazi wanaoishi maeneo ya ndara kaunti ndogo ya Voi.
Aidha Mwandawiro amesema jamii za ndara zimeishi kwa miaka mingi Katika eneo hilo akishangaa kuwa sasa wanatakiwa kutoka maeneo hayo bila na kupewa mahali pengine mbadala pahamia.
Wakati huohuo katibui huyo ameitaka serikali ya kitaifa kupitia afisi ya kaunti kamishna  Rodah Onyancha kushirikiana na wizara yake ili kutatua Changamoto hizi kikamilfu.
 

  

Latest posts

Nadal Atinga Nusu Fainali Ya Michuano Ya Wimbledon

Clavery Khonde

Raheem Sterling Akubali Kujiunga Na Chelsea

Clavery Khonde

Waziri Chelagui Awahimiza Vijana Kujiunga Na Vyuo Vya Kiufundi

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi