Koome Awapa Ilani Mawakili

Huku nchi ikijiandaa kupiga kura katika muda wa siku 75, katika kile kinachojidhihirisha kuwa mchujo mkali wa kumrithi rais Uhuru Kenyatta, uwezekano wa mchuano huo kuishia katika Mahakama ya Juu uko hai.

Jaji Mkuu Martha Koome, ambaye pia ni rais wa mahakama ya upeo, ambayo ina mamlaka ya kipekee ya malalamiko ya uchaguzi wa urais, amewapa ilani mawakili na washtakiwa ambao wangetaka kushtaki masuala kama hayo katika mahakama ya maoni ya umma.

Also Read
Saburi Atawazwa Na Wazee Wa Kaya Kuwania Ugavana Kilifi

Maagizo yaliyomo katika toleo maalum la gazeti la Kenya la Mei 5, 2022 walalamikaji katika ombi la uchaguzi wa urais na mawakili wao wasitoe maoni yao kuhusu ubora na ubaya wa masuala kama hayo, au hata kutabiri matokeo ya malalamiko kama hayo, hadi Mahakama ya upeo itakapo toa uamuzi wake kuhusu matokeo ya kura za urais.

Also Read
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaungana Kwale

Kifungu cha 140 cha Katiba kinaruhusu watu ambao hawajaridhika na matokeo ya uchaguzi wa urais kuwasilisha malalamiko ya kupinga uchaguzi wa rais mteule ndani ya siku saba tangu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.

Also Read
Jaji Mkuu Koome Azindua Baraza La Kitaifa La Utawala Na Haki

Mahakama ya Juu inabidi ndani ya siku 14 kusikiliza na kuamua maombi hayo na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.

Iwapo Mahakama ya Juu itaamua uchaguzi wa rais- mteule kuwa si halali uchaguzi mpya utafanywa ndani ya siku sitini baada ya uamuzi huo.

  

Latest posts

Ofisi Ya Msajili Yawashirikisha Washikadau Kwenye Msafara Wa Amani Pwani

Ruth Masita

Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Viwango Vya Elimu Jomvu

Ruth Masita

WRC Safari Rally Kuandaliwa Naivasha

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi