KRA Yanasa Sabuni Ya Maghendo Vanga

Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru nchini (KRA) imenasa magunia 65 ya sabuni ya unga iliyoingizwa humu nchini kinyume cha sheria kutoka Tanzania, katika eneo la  Vanga kwenye mpaka wa  Kenya na Tanzania.

Kulingana na mkurugenzi wa mamlaka hio eneo la pwani Joseph Tonui ni kuwa serikali ingepoteza jumla ya shilingi  96,354 katika ushuru wa forodha ikiwa ingekosa kukamata bidhaa hio kabla ya kusambazwa kwa wateja sokoni

Also Read
George Kithi aahidi kujenga kiwanda cha matunda kaunti ya Kilifi akichaguliwa kuwa gavana

Maafisa wa Forodha huko Lunga inaaminika walipokea  taarifa kwamba jamaa mmoja alikuwa  akipakua bidhaa hizo  nyumbani kwake eneo la Vanga na timu ya wakala ikiongozwa na maafisa wa KRA ilikimbia hadi kwenye eneo hilo  na kufanikiwa kunasa sabuni ya unga ndani ya nyumba na duka, vyote vinamilikiwa na mtuhumiwa.

Also Read
Wavuvi Vanga Watakiwa Kuwa Na Maadili

Mmiliki wa duka hakuweza kutoa hati ya kibali cha sabuni hio hali iliyosababisha  maafisa kukamata bidhaa hizo na kuzisafirisha hadi kwa Ghala maalum kwa ulinzi kusubiri  hatua zaidi za kisheria.

Kuzuiliwa kwa bidhaa hizo zenye uzito wa kilo 795, kunajiri  siku chache baada serikali kuagiza msako mkali dhidi ya biashara ya bidhaa ghushi  katika eneo la mpakani   Kaunti ya Kwale.

Also Read
‘Sikai chini. Wachana na mimi

Wiki iliyopita, timu ya mashirika ya serikali ikiongozwa na mshirikishi wa kanda ya pwani  John Elungata, ilifanya mikutano ya usalama wa kikanda na viongozi wa eneo hilo na wafanyabiashara wa Lunga Lunga, Vanga na Shimoni ambapo walikubaliana  kuwa wote watashirikiana kwa karibu kukomesha biashara ya magendo eneo la mpakani.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi