Wakaazi wa Bombolulu wamelalamikia kutokuwepo kwa matuta ya barabara kuu ya Mombasa -Malindi hatua ambayo inaweka maisha yao hatarini kutokana na magari ambayo hupita kwa mwendo wa kasi katika barabara hio.
Wakaazi hao wanasema kwamba kwa siku za hivi maajuzi kumekuwepo na ongezeko la visa vya ajali katika eneo hilo huku wengi walioojeruhiwa wakiwa ni wanafunzi ambao huvuka barabara hio wanapoenda shuleni.
Wakizungumza na Pwani Fm wakaazi hao waliojawa na ghadhabu wametoa makataa kwa mamlaka ya usimamizi wa barabara nchini KeNHA kuweka matuta katika barabara hio kwa kile wanachokitaja kuchoshwa na kushuhudia visa vya ajali ambavyo hufanyika kila uchao katika eneo hilo.