Luke Shaw adai refa alidinda kutoa Penalti kwa hofu ya kuzuka gumzo

Luke Shaw adai refa alidinda kutoa Penalti kwa hofu ya kuzuka gumzo
Beki wa Manchester United Luke Shaw amedai kuwa refari wa mechi kati yao na Chelsea Stuart Atwell alikataa kuipa Manchester united Penalty kwa kuhofia mjadala mkali ambao ungezuka endapo angebadilisha uamuzi wake wa awali.
Marefari waliokuwa wanasimamia VAR walimwagiza refarii wa mechi kuangalia tena tukio ambalo mchezaji wa Chelsea Hodson Odoi alionekana kunawa mpira katika eneo la hatari licha ya wao kupendekeza kuwa tukio hilo lilikuwa penalty.
Luke shaw amedai alimsikia Atwell akimwambia nahodha wa united Harry Maguire kuwa endapo angetoa penalty angezua mjadala mkali baadaya mechi.
Vile vile mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwaclub yake alifaa kupata penalti.
Mechi kati ya Manchester united na Chelsea imeishia sare huku Manchester united wakiendelea kuweka rekodi mbaya dhidi ya vilabu sita vikubwa ndnai ya Ligi ya Epl.

  

Latest posts

PSG Kumtema Neymar

Clavery Khonde

WRC Safari Rally Kuandaliwa Naivasha

Clavery Khonde

Bayern Munich Wakamilisha Usajili Wa Sadio Mane

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi