Magari 315 Kupigwa Mnada Katika Bandari Ya Mombasa

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA inaongoza shughuli ya kuyapiga mnada magari 315 na bidhaa nyingine katika bandari ya KPA hapa mjini Mombasa hii leo na hapo kesho. 

Mshirikishi wa mamlaka hiyo eneo la Kusini Joseph Tunui amesema bidhaa nyingine ni ambazo ziko ndani ya makasha 223 , miongoni mwa bidhaa hizo ni nguo a viatu zilizotumiwa.

Wakati huo huo amesema wananchi wanaotaka watapewa nafasi ya kushiriki kwenye mnada huo.

Shughuli hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia masharti yote ya kuthibiti  maambukizi ya korona.

KRA inalenga kukusanya kati ya shilingi milioni 150 na 200 kutoka kwa mnada wa bidhaa hizo ambazo zimekawia bandarini baada ya kupitisha muda unaofaa wa bidhaa zilizoagizwa nchini kuondolewa, ikiwemo waagizaji kushindwa kulipa kodi ya kiwango kilichostahili.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi