Mahakama Kuu Mombasa Yatoa Amri Ya Kufukuliwa Kwa Mwili Wa Anverali Nazerail

Mjane wa marehemu mfanyabiashara Anverali Nazerail Kiran Nazerali, binti yake Mahek Fatima mwenye umri wa miaka 20 na bintiye wa pili Nurjehan Nazerali wa miaka 18 walipata afueni baada ya mahakama kuu ya Mombasa kutoa amri ya kusimamisha shughuli ya kufukuliwa kwa mwili ili uchunguzi wa maiti ufanyike.

Jaji Anne Apondi Ong’injo kwa muda aliidhinisha familia ya marehemu amri ya kukaa hadi kesi hiyo isikizwe na kuamuliwa mbele ya mahakama.

Familia ya walioachwa kupitia mawakili wao Mohammed Balala na Sborne Lijoodi walikuwa wamehamia mahakama kuu kupinga uamuzi wa mahakama ya chini katika ombi la afisi ya upelelezi wa jinai katika eneo la pwani la kuufukua mwili wa Nazerali kwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake.

Mawakili hao walikuwa wamehamishwa hadi mahakama kuu chini ya cheti cha dharura takriban saa tatu baada ya agizo kutolewa la kuufukua mwili huo ambao ulizikwa miezi miwili iliyopita katika makaburi ya Khoja Shia ithnaasheri kaunti ya Mombasa.

Jaji Ong’injo aliamuru kusimamishwa kwa uamuzi wa Hakimu Mkaazi Mwandamizi wa Mombasa Vincent Adet akimpendelea afisa wa CID wa eneo hilo kuufukua mwili wa marehemu hadi amri nyingine zitakapotolewa.

Hata hivyo, mjane wa marehemu mfanyabiashara akiwa na mabinti zake wawili waliapa kupigania mwili wa marehemu ili wasisumbuliwe na kukaa kwa amani wakisema kuwa mazishi hayo yalifanyika kwa kufuata mafundisho ya Kiislamu.

  

Latest posts

Mvurya Ataka Maafisa Wa Idara Na Mashirika Ya Serikali Kuhusu Maendeleo Zishirikishe Serikali Za Ugatuzi

Ruth Masita

Wanawake Wajasiriamali 450 Wanufaika Na Mafunzo Ya Kibiashara Mombasa

Ruth Masita

Mahakama yamwachilia mbunge wa Sirisia John Walukhe kwa dhamana ya shilingi milioni kumi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi