Makala maalum: Wanawake na Mamlaka.

PRODUCED BY:RUTH MASITA

Kutokuwepo na usawa wa kijinsia na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana ni ukatili unaopaswa kushughulikiwa sasa.

Wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto katika kuafikia malengo yao hasa pale wanapotafuta haki zao za uwakilishi katika nafasi za uongozi kutokana na mfumo wa dume uliojengeka miongoni mwa jamii kuanzia ngazi ya familia.

Sehemu kubwa ya jamii yetu hapa nchini, imekuwa ikimwangalia mwanamke kwa mtazamo tofauti unaomuashiria kuwa kiumbe kisichoweza kuleta maendeleo katika jamii.

Katika makala haya ninafanya utafiti wa kufahamu jinsi wanawake wanavyojizatiti kuhakikisha wanamiliki mamlaka na kujikwamua kutokana na dhana hizo potofu kuwa hawawezi.

Also Read
Siasa Za Msambweni Zapamba Moto

Hii leo nazungumza na mama Hamisa Zaja ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa wengi hasa wale wanaoishi na changamoto mbalimbali za ulemavu.

Bi. Zaja amekuwa akituzwa na kazi yake nzuri kwa ajili ya kuweza kubadilisha maisha ya watu tofauti tofauti.

Ili kufanikiwa katika uongozi ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anafanya mambo kadha wa kadha kama anavyofanya Bi. Zaja hasa wakati huu wa ujio wa janga la Covid 19 ambapo alitengeza maski za kuwawezesha watu wanaoishi na ulemavu wa kutosikia na kuzungumza.

 

Bi. Zaja kulia ,aliyetengeza barakoa spesheli za watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia.

 

Wakati huo huo wanawake hupitia changamoto wanapotekeleza majukumu maalum na yaliyo na mguso mkubwa katika jamii.

Also Read
Chama Cha PAA Chazidi Kufungua Afisi Asema Mwaganda

Baada ya kuishughulikia jamii bila kutilia maanani changamoto anazopitia Bi. Zaja bado hajakata tamaa.

Ananieleza azma yake ya kuwania kiti cha uwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Mombasa.

Ni dhahiri kwamba mwanamke akipatiwa fursa na kujengewa mazingira ya kuondoa vikwazo vinavyochangia kumfanya ashindwe kufikia kuwa viongozi, anaweza kuwa kiongozi mzuri katika nafasi aliyopata.

Ni kipi tunatarajia kutoka kwako endapo utafaulu.

Anatoa wito kwa wanawake wengine ambao wamekuwa waking’ang’ania nafasi za uongozi kwamba wasikate tamaa.

Pia nafanya juhudi za kutaka kuzungumza na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la maendeleo ya akina mama Afia Rahma.

Also Read
Bunge la seneti latishia kumchukulia hatua Gavana Joho iwapo atandelea kususia mwaliko wa kamati ya uchukuzi

Kwa sababu ya changamoto zisizoepukika nazungumza naye kwa njia ya simu.

Ananieleza changamoto akina mama wanazopitia, mikakati waliyoitekeleza sawa na mapendekezo yao kwa serikali.

Ubaguzi dhidi ya wanawake unatokana na ubinafsi.Tunaweza kuinuka dhidi ya kila aina ya ubaguzi tunaorushiwa na kuongoza si kaunti hii pekee bali nchi nzima.

Hakuna tatizo lolote katika kuwa na gavana wa kike, mbunge, seneta au hata kiongozi wa taifa.

Kwa niaba ya mhariri wetu Joshua Chome, nimekuwa mtayarishi na msimulizi wako Ruth Masita.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi