Mali Inasukumwa Kubuni Serikali ya Utawala wa Kiraia

Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana, amesema viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanatarajia kufanikiwa kubuniwa kwa serikali ya utawala wa kiraia imebuniwa nchini Mali katika kipindi cha siku kadhaa. Alisema hayo baada ya mashauriano baina ya viongozi wa kanda hiyo na jeshi lililotwaa mamlaka nchini Mali mwezi uliopita. Akufo-Addo alisema shirika la Ecowas, litaondoa vikwazo serikali ya kiraia itakapobuniwa nchini Mali. Viongozi wa shirika la Ecowas walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mashauriano kuhusu mzozo wa kisiasa unaokabili Mali.  Viongozi wa jeshi la Mali pamoja na wawakilishi wa umoja wa mataifa na jumuiya ya Afrika, pia walihudhuria. Viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanahofu kwamba hali ya usalama nchini Mali huenda ikadorora na kuhujumu juhudi za kukabiliana na wanamgambo nchini humo. Siku ya jumamosi, chama cha upinzani cha M5-RFP kilikataa pendekezo la jeshi la mchakato wa mpito wa miezi 18

Also Read
Rais wa Mali aliyepinduliwa madarakani aaga dunia

Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana Anataka serikali ya utawala wa kiraia kubuniwa Mali

  

Latest posts

Abiria aaga dunia ndani ya ndege iliyotoka New York

Tima Kisasa

Wabunge wapya kupewa hamasa ya shughuli za bunge alhamisi

Joshua Chome

Maafisa nchini Somalia mashakani

Tima Kisasa

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi