#KurunziYaPwani
Watu kumi na watano wamedhibitishwa kufariki kutokana na mapromoko Venezuela katika magharibi mwa jimbo la Mérida.
Barabara za vitongoji vilivyo milimani iligeuzwa kuwa mito yenye nguvu baada ya mvua kubwa kukumba eneo la Andes.
Maafa zaidi yalitokea katika mji wa Tovar ambako mto Mocotíes ulivunja kingo zake baada ya saa nyingi za kunya kwa mvua hiyo.
Maafisa katika eneo hilo wanasema kuwa kituo cha nguvu za umeme Tovar imeharibiwa ,wakaazi wakikosa umeme na mwasiliano ya simu.
Hii sio mara ya kwanza kwa bonde la Mocotíes kukumbwa na maporomoko.
Mwaka 2005 zaidi ya watu 40 waliaga dunia na wengine wengine wengi kupotea katika eneo hilo mito kadhaa ilipofurika.