Maseneta wateta juu ya kupanda kwa bei ya mafuta

Waziri wa kawi Charles Keter na mwenzake wa mafuta na madini John Munyes leo wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya seneti ya kawi kuelezea sababu ya kuendelea kupanda kwa bei za mafuta.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei aliwasilisha ombi mbele ya seneti akitaka kamati hiyo kuwahoji wawili hao pamoja wa washikadau wengine katika sekta ya kawi wakiwemo uongozi wa mamlaka ya kutathmini bei ya mafuta na kawi kabla ya kuwasilisha mbele ya bunge maelezo kamili.

Also Read
Wakulima Kifili walalamika kwa ukosefu wa wataalam wa kilimo mashinani
Also Read
Jeshi La KDF Lalimbikiziwa Sifa Wakati Wa Siku Ya KDF

Maswali sawa na hayo yanatarajiwa kuibuliwa katika bunge la kitaifa, wakati ambapo wabunge watakuwa wakiregelea vikao vya hii leo.

Haya yanajiri huku shughuli kadhaa zikilisubiri bunge litakaporegelea vikao vyake hii leo baada ya mapumziko.

Also Read
Mamlaka ya mazingira NEMA yafunga migodi siku moja baada ya wawili kufariki kaunti ya Kwale

Mbali na suala la mafuta, kamati ya utekelezwaji wa katiba ikiongozwa na Jeremiah Kioni inatarajiwa kuwasilisha hoja ya kubuni wadhfa wa waziri mkuu na manaibu wake wawili.

  

Latest posts

Viongozi wa Kilifi Waunda Kamati Ya Kutatua Mizozo ya Ardhi

Ibrahim Nyundo

Seneta Wa Lamu Afikishwa Mahakamani

Clavery Khonde

Lalama Za Ongezeko La Ajali Vuga

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi