Mashirika Ya Kijamii Yaeleza Dosari Za Uchaguzi Mkuu Wa Tarehe 9 Agosti

Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali katika kaunti ya Mombasa kwenye tahmini yao yamedai kuwa uchaguzi wa tarehe 9 mwezi huu ulighubikwa na dosari za kiusalama na ufisadi.

Kwenye mkao na wanahabari mashirika  hayo yamelalamika kufunguliwa kuchelewa kwa vituo vya uchaguzi, kuhongwa kwa wapiga na utumizi wa kiholela wa bunduki na baadhi ya wanasiasa kuwa miongoni mwa vitu vilivyotishia wakaazi kufanya uchaguzi wa amani.

Also Read
Mataifa ya Asia Yaongoza Katika Uchafuzi wa Hewa Duniani

Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano huo wa mashirika ya kijamii nchini Zedekiah Adika mashirika hayo yametaka uchunguzi wa haraka kufanywa kuhusu wanasiasa waliotumia bunduki zao kiholela sawa na jinsi swala zima la uchaguzi lilivyotekelezwa.

Also Read
Human Rights Watch yashutumu vikosi vya usalama Misri

Kwa upande wake afisa wa maswala ya dharura katika shirika la kijamii la MUHURI Francis Auma amedai kwamba mashirika hayo yako na ushahidi wa wanasiasa wakitoa hongo kwa wapiga kura na vurugu katika maeneo mbalimbali ya kaunti hii.

  

Latest posts

Watoto Wanaotelekezwa Wako Hatarini Ya Kujiunga Na Makundi Ya Kihalifu Asema Hakimu Nabwana

Clavery Khonde

Rais aahidi kukomesha aibu ya njaa nchini

Joshua Chome

Mradi Wa Unyunyiziaji Mashamba Maji TanaRiver Waimarishwa

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi