Mbuge wa Ganze Teddy Mwambire anaendelea kupigania hoja yake ya kuwajengea shule maalum wasichana waliopata ujauzito na kulazimika kuacha shule katika eneo hilo.
Katika mahojiano kwa njia ya simu Teddy amesema tayari amezindua shule ya upili Bamba girls yenye itakua ikisajili wanafunzi walioacha shule kutokana na mimba za mapema na wako na mikakati ya kujenga Zaidi ya shule 6 katika eneo bunge hilo ambazo sitakuwa ni za wasichana pekee.
Hata hivyo Ameongeza kuwa Nia yake ni kuhakikisha shule zote katika eneo hilo zinakuwa za jinsia moja na pia za malazi ambapo kulingana na yeye hali hiyo itaweza kupunguza mimba za mapema katika eneo hilo.