Mkuu Wa DCI George Kinoti Ahukumiwa Kifungo Cha Miezi Minne Kwa Kudharau Mahakama

Mkuu wa Idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne katika gereza la Kamiti kwa kosa la kudharau mahakama.

Hii ni baada ya kukosa kutii amri za mahakama zilizomtaka kurejesha bunduki alizompokonya mgombea urais wa 2022 Jimmy Wanjigi.

Also Read
Wanaokiuka Kanuni Za Afya Kukabiliwa Kisheria Asema Elungata

Kinoti anatarajiwa kujisalimisha gerezani ndani ya siku 7 bila kufanya hivyo, kiongozi wa mashtaka ya umma  ameagizwa kutoa hati ya kukamatwa kwake.

Mkurugenzi wa upelelezi wa Jinai, George Kinoti, alipewa siku 30 mapema 2021 na mahakama kuu jijini Nairobi kurejesha bunduki za mfanyabiashara Jimmy Wanjigi, kama ilivyoagizwa mwaka wa 2019.

Also Read
Jamaa Aliyehukumiwa Miaka 60 Jela Kwa Ulanguzi Wa Wanawake Alalamikia Hukumu Hio

Makataa ya DCI kutii maagizo hayo ilikuwa Machi 25, 2021.

Mnamo Juni 2019, Jaji Chacha Mwita aliamua kwamba Serikali ilitenda bila busara kwa kunyakua bunduki za Wanjigi ilhali bado alikuwa na leseni halali.

Also Read
Balozi wa Italia auawa DRC

Mnamo 2017, polisi walinasa bunduki saba kutoka kwa nyumba ya mfanyabiashara huyo huko Malindi.

 

  

Latest posts

Nadal Atinga Nusu Fainali Ya Michuano Ya Wimbledon

Clavery Khonde

Raheem Sterling Akubali Kujiunga Na Chelsea

Clavery Khonde

Waziri Chelagui Awahimiza Vijana Kujiunga Na Vyuo Vya Kiufundi

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi