Mombasa Inaupungufu Wa Wauguzi 500 Asema Katibu Wa Wauguzi

Sasa Imebainika kuwa kaunti ya Mombasa inaupungufu wa wauguzi wa afya 500.

Haya ni kwa mujibu wa katibu mkuu wa muungano wa wauguzi kaunti ya Mombasa Emily Mursoi.

Katika mahojiano ya kipekee na pwani fm kwa njia ya simu Mursoi amedokeza kuwa upungufu huo umetokana na baadhi ya wahudumu wa afya kustaafu huku wengine wakiajiriwa katika kaunti tofauti.

Wakati huo huo ameonyesha matuamaini ya kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa itatimiza ahadi ya kuhakikisha kila tarehe tano wanawalipa mishahara yao.

Haya yanajiri baada ya wauguzi hao pamoja na madaktari kusitisha mgomo wao baada ya kulipwa mshahara wao wa miezi miwili waliokua wakiidai serikali ya kaunti ya Mombasa.

  

Latest posts

Gor Mahia Wapiga Kalamu Harrison na Benchi Lake La Kiufundi

Clavery Khonde

Sportpesa Yatoa Vifaa Vya Matibabu Kilifi

Clavery Khonde

Hospitali Za Kibinafsi Kukataa Huduma Za NHIF Mwezi Ujao

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi