Msako Dhidi Ya Mabaa Wafanywa Kwale

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeanzisha oparesheni ya kuwasaka wamiliki wa baa na vilabu vya pombe walio na tabia za kuwaficha wateja wao kinyume na masaa yaliyoidhinishwa na serikali msimu huu wa janga la Corona.
Kamishna wa Kwale Joseph Kanyiri amesema kwamba maafisa wa polisi watalazimika kutumia nguvu zaidi ili kuwakabili wamiliki hao wa baa wanaokiuka masharti ya wizara ya afya ya kukabiliana na maambukizi.
Wakati uohuo amewataka machifu kuhakikisha mangwe za pombe ya mnazi zinafuata kanuni za kuthibiti Corona
Kauli yake inajiri baada ya baadhi ya wamiliki wa Mabaa kupuuza masharti ya masaa ya kuuza pombe yao hatua ambayo ameitaja kinyume cha sheria.
 

  

Latest posts

Nadal Atinga Nusu Fainali Ya Michuano Ya Wimbledon

Clavery Khonde

Raheem Sterling Akubali Kujiunga Na Chelsea

Clavery Khonde

Waziri Chelagui Awahimiza Vijana Kujiunga Na Vyuo Vya Kiufundi

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi