Hit maker wa ‘Jerusalama’ Master KG amedhibitisha kuwa hakuna msaani aliyelipwa mgao wa fedha unaotokana na wimbo huo.
Kupitia taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari, MasterKg amedai kuwa usimamizi wake umekuwa katika mazungumzo na Nomcebo Zikode toka mwezi June 19 lakini kufikia sasa bado hawajaafikiana.
Kulingana na taarifa, wawili hao walikuwa wameafikiana mgao wa 50-50 kwenye mapato ya wimbo wa ‘Jerusalema lakini taarifa zilizopo ni kuwa Nomcebo alitaka mgao wa asilimia 70 tofauti na mkataba ulivyo.
Vilevile,Master Kg amedai kuwa Nomcebo alifanya world wid tour ya Jerusalama bila ya kumhusisha yeye kama muimbaji mwenza wa kibao hicho.
Aidha Nomcebo amedai kuwa amekuwa akitengwa na kufikia sasa hajapata mgao wowote wa fedha zinazotokana na kibao hicho kinachotajwa kuwa world wide hit.