Mikakati dhabiti kuhusu mipango maalum inaendelea kuwekwa na serikali ili kuhakikisha afya ya kiakili inayotokana na msongo wa mawazo kwa walimu wakuu shuleni unakabiliwa.
Akizungumza na wanahabari katika kongamano la walimu wakuu hapa Mombasa mshauri wa maswala ya afya katika afisi ya rais Dkt. Frank Njenga amesema kuwa kulingana na majukumu ya walimu wakuu shuleni imewalazimu kuwa na umuhimu wa kuhakikisha afya yao inalindwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu katika shule za upili KESSHA Kahi Indimuli amesema kuwa wanaelewa changamoto zinazosababisha msongo wa mawazo miongoni mwa walimu shuleni, hivyo wanashirikiana na washikadau husika kutoa mpango wa hamasa ili kufahamu jinsi ya kuikabili hali hiyo
Haya yamejiri kwenye kongamano la walimu linaoendelea hapa Mombasa ambapo inatarajiwa kukamilika hii leo.