Mtalii mmoja nchini Uganda amekanyagwa na ndovu hadi kufa katika mbuga ya wanyama ya Murchison Falls na kushuka kwenye gari alilokuwa akisafiria.
Marehemu, ni raia wa Saudia, alikuwa akipita kwenye mbuga ya taifa ya wanyama hiyo iliyo katika jiji la Arua pamoja na wenzake wakati waliposimama kujisaidia.
Kundi la ndovu waliokuwa na hasira lilimvamia marehemu,ambaye alikuwa amekwenda mbali zaidi ya gari lilpokuwa na hakuweza kurejea.
Maafisa wa mbuga ya wanyama hiyo wamedhibitisha tukio hilo na walisema upelelezi unaendelea.
Aidha hatua zinachukuliwa kuzuia matukio ya aina hiyo kutokea tena.
Mashmabulio ya wanyama yamekuwa yakiripotiwa katika kipindi cha nyuma katika mbuga za wanyama za Uganda.