Museveni Alegeza Masharti Ya Kudhibiti Korona Licha ya Maambukizi Kuongezeka

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kulegezwa zaidi kwa masharti ya kuthibiti msambao wa ugonjwa wa Korona, licha ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi nchini humo. Wizara ya afya nchini Uganda inasema ongezeko hilo linatokana na kupuuzwa kwa agizo la kutangamana na kuvaa barako hasa katika maeneo ya umma. Rais Museveni amesema masharti hayo hayawezi kudumishwa milele, akisema uchumi wa nchi hiyo umeathirika mno kutokana na janga hilo. Aidha, alisema serikali ya nchi hiyo itafungua mipaka kwa watalii huku raia wa nchi hiyo waliobainishwa kuambukizwa virusi vya Korona wanaorejea nyumbani wakishauriwa kujitenga. Makanisa pia yamekubaliwa kuendelea na ibada lakini ni waumini 70 pekee watakaoruhusiwa kanisani kwa wakati mmoja.

Also Read
Rais Yoweri Museveni wa Uganda asema Uchumi wa Taifa hilo Umeathirika mno na Covid 19
  

Latest posts

Rais wa Somalia na Waziri Mkuu watatue tofauti zao

Tima Kisasa

Jaribio la Mapinduzi Sudan

Tima Kisasa

Chama cha Putin chaongoza Urusi

Tima Kisasa

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi