Mvuvi mmoja eneo la Watamu kaunti ya Kilifi amethibitishwa kufariki baada ya kuzama baharini alipokuwa akivua samaki jana asubuhi.
Akithibitisha kifo hicho mwenyekiti wa usimamizi wa fuo za bahari BMU eneo hlilo Athman Mwambire amesema marehemu kwa jina Kazungu Mwangale alikuwa na wenzake wakivua kabla ya boti lao kupigwa na mawimbi na kuzama.
Mwambire amesema kuwa Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi huku akiwaonya wavuvi dhidi ya kwenda baharini wakati huu bahari imechafuka.