Mwanakandarasi asimamishwa Kilifi

Mwakilishi wa wadi ya Malindi kaunti ya Kilifi David Kadenge ametamaushwa na hatua ya mkuu wa elimu katika kaunti ndogo ya Malindi pamoja na mkuu wa wilaya kwa kumsimamisha mwanakandarasi aliyekuwa akiendeleza ujenzi wa hospitali katika eneo la Kisumu Ndogo.

Also Read
Lalama Za Barabara Mbovu Junda Mombasa

Akizungumza na wanahabari katika majengo ya   bunge la Kaunti hiyo Kadenge amesema kuwa tayari mazungumzo kati ya wanakijiji pamoja na usimamizi wa shule hiyo ulikuwa umefanyika katika afisi ya gavana jambo ambalo lilipelekea mwanakandarasi huyo kupewa kazi ya kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo .

Also Read
Ann Kananu Apishwa Kuwa Gavana wa Nairobi

Kadenge amesema kuwa bado hajajua sababu kuu ya wawili hao kuchua hatua ya kusimamisha ujenzi huo huku akikisia swala la vita vya kisiasa jambo ambalo limempelekea kusema kuwa madhumuni ya mradi huo ni kufaidi wanajamii wa eneo hilo.

Also Read
Kilio Cha Umeme Malindi

Aidha, Kadenge amesema kuwa sasa anatarajia kufanya mazungumzo na gavana wa kaunti hiyo Amason Jefa Kingi hapo kesho ili kubaini kiini cha kusimamishwa kazi hiyo kwani bado hajapata mwafaka wa swala hilo kutoka kwa waziri wa afya.

  

Latest posts

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Pwani Wahamasisha Wenzao Kuhusu Amani

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi