Mwanaume mmoja raia wa Australia anashtakiwa kwa kosa la kumteka nyara mtoto wa miaka minne Cleo Smith, ambaye aliokolewa baada ya siku 18.
Terence Darrell Kelly mwenye umri wa miaka 36, amefikishwa mahakamani katika mji wa Carnarvon, akishtakiwa kumchukua mtoto kwa nguvu au kwa ulaghai mtoto ambaye yuko chini ya miaka 16 .
Tangu Oktoba 16, Cleo Smith alipotea toka kwa familia yake wakati wakiwa katika kambi ya familia na kutafutwa sana.
Cleo alipatikana na polisi kwenye nyumba iliyokuwa imefungwa huko Carnarvon siku ya Jumatano.
Mtoto huyo sasa ameungana na wazazi wake ambao walikuwa wamemtafuta mpaka kukata tamaa.
Mamlaka inasema bwana Kelly hana uhusiano wowote na familia ya Smith, yaani walikuwa hawajuani.