Mwaniaji Wa Kiti Cha Ubunge Mvita Mohammed Machele Azindua Manifesto Yake

Mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Mvita hapa Mombasa Mohammed Machele amewataka wakaazi wa mvita kumchagua ili aweze kutekeleza yote aliyoyataja kwenye manifesto yake.

Akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Emirates hapa Mombasa, Machelle ameeleza yale ambayo atayapa kipaumbele ni pamoja na Elimu, biashara, michezo na afya.

Kadhalika Machele, ametumia fursa hiyo kumuombea kura kinara wa muungano wa Azimio la umoja One Kenya Raila Odinga, ambapo amewahimiza wakaazi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi na kupiga kura siku ya tarehe 9.

Wakati huo huo seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki amewataka wakaazi wa Mvita kumuunga mkono Machelle huku akimtaja kama kiongozi mchapa kazi na mnyenyekevu kwa wananchi.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi