Mwidema ashinda gavana wa sasa na wa zamani

Andrew Mwidime mgombea huru kwenye uchaguzi wa ugavana kaunti ya Taita Taveta  aliwashinda wapinzani wake 13 akiwemo  gavana anayeondoka Granton Samboja na gavana wa zamani John Murutu.

Mwadime mbunge anayeondoka wa Mwatate  alipata kura 49,901 huku gavana wa sasa Granton Samboja wa Jubilee akipata kura takriban nusu  ya alizozoa ambazo ni 23,703.

Also Read
Polisi Voi Wachunguza Kifo Tatanishi Cha Mwanamume Mmoja

Gavana wa zamani John Mrutu wa UDA alichukuwa nafasi ya tatu kwa kupata kura 13,865  huku senata wa zamani Dan Mwazo akipata kura 11,543.

Mwadime anakuwa gavana wa pili kuchaguliwa kama mgombea huru baada ya kutangazwa ushindi wa  Kawira Mwangaza aliye pia wania waadhifa huo kaunti ya Meru  kama mgombea huru na kumshinda  gavana anayeondoka Kiraitu Murungi.

Also Read
Wakaazi Wa Kwale Wahimizwa Kusirikiana Na Serikali

Wakaazi wa eneo la kaunti ya Taita Taveta kila uchaguzi wamekuwa wakimchagua gavana mpya.

Mwezi Machi  alikihama chama cha ODM baada ya kubainika kwamba angeshiriki kura ya mchujo ya kuwania waadhifa huo na wanasiasa Thomas Mwakwida na Racheal Mwakazi.

Also Read
Wauguzi Taita Taveta Kusitisha Mugomo

Jonnes Mwaruma  wa ODM ndiye senata wa eneo hilo kwa kupata kura elfu 39,142  huku Lidya Haika wa UDA  akipata kura 38, 363 na sasa atashikilia waadhifa wa mbunge wa kaunti hiyo.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi