NACADA yapigwa jeki kupitia ujenzi wa kituo Methadone Miritini

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Usalama na Utawala wa kitaifa Peter Mwathi ameahidi kutolewa fedha zaidi kuelekeZzwa kwenye ujenzi wa kituo cha Matibabu ya waraibu wa dawa za kulevya  cha Miritini.

Kituo hicho kinatarajiwa kusaidia kukabiliana na hatari ya utumiaji wa dawa za kulevya katika Mkoa wa Pwani. Mombasa imetajwa kuongoza katika utumizi wa dawa za kulevya katika mkoa wa Pwani. Hii ndio iliyomsukuma raisi Uhuru Kenyatta kutoa maagizo ya ujenzi wa Kituo cha Matibabu na Ukarabati cha Miritini.

Also Read
UNESCO yaamua Kiswahili kuadhimishwa duniani kila tarehe 7 mwezi wa Julai
Also Read
Kwale Yaweka Mikakati Yakukabili Athari Za Ukosefu Wa Mvua

Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa NACADA Victor Okioma, mgao wa rasilimali umekuwa changamoto kubwa katika kufanikisha mradi huo hili likisababisha Kamati ya Bunge ya Usalama na Utawala wa Kitaifa kuanzisha mpango wa kutafuta ukweli juu ya lalama hizo.

Also Read
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa Achiliwa kwa dhamana

Mradi ukikamilika  utakuwa na uwezo wa kukubali walevi mia mbili mbali na kutoa huduma za wagonjwa wa nje. Kituo hicho pia kinatarajiwa kutoa ufundi wa kiufundi kwa wale walio katika matibabu kabla ya kuruhusiwa kujiunga tena na jamii.

  

Latest posts

Wafanyibiashara Katika Soko La Malindi Walalamikia Uchafu na Uvundo.

Sylvester Chibero

Wakenya Wametakiwa Kuwa Waangalifu Wakati Wanapoabiri Magari Msimu Huu Washerehe.

Sylvester Chibero

Tutashamiri Kwenye Mashindano Ya Mwaka Huu Ya Tong-IL Moo Do Asema Master Mwakio

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi