Naibu rais Dkt William Ruto ajibu madai kuwa anamiliki kipande kikubwa cha ardhi Laikipia

Naibu wa rais William Ruto amewataka wale wanaodai kuwa ana kipande kikubwa cha ardhi katika kaunti ya Laikipia kukichukua na kukikabidhi kwa maelfu ya wakazi ambao wanatoroka eneo hilo kutokana na ukosefu wa usalama.

Ruto alisisitiza haja ya kukabiliana ipasavyo na mapigano yanayoshuhudiwa katika eneo hilo ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu wanane.

Also Read
Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema serikali imejitolea kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya

Wakati huo huo naibu wa rais alisisitiza msimamo wake kuwa inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai anapaswa kukoma kujihusisha na siasa na kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Also Read
Kilimo cha Mpunga Vanga chapigwa Jeki na Serikali

Akiongea alipokutana na viongozi wa mashinani kutoka eneo bunge la Narok kusini katika makazi yake ya  Karen,Ruto alidai kuwa ghasia zinazozidi kushuhudiwa katika eneo la  Laikipia zimedhihirisha kasoro zilizoko katika huduma ya usalama nchini.

Juma lililopita waziri wa usalama wa taifa Fred Matiangi alifika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu usalama wa taifa na kuwaambia wabunge kuwa Ruto analindwa na maafisa 257 wa usalama.

Also Read
Wakaazi Wa Kaunti Ya Tana River Waonywa Dhidi Ya Kula Mizoga Ya Ng'ombe

Matiang’i alidai kuwa Ruto anamiliki hekta 6,073 za ardhi katika eneo la ADC Laikipia Mutara ranch.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi