Naibu rais Dkt William Ruto asema yuko tayari kwa mazungumzo ya maridhiano na rais

Naibu Rais Dr. William Ruto amesema yuko tayari kwa mazungumzo kuhusu maridhiano baina yake na Rais Uhuru Kenyatta bila masharti yoyote.

Akiongea wakati alipokutana na ujumbe kutoka Kandara, kaunti ya Murang’a, Naibu Rais alisema anamheshimu Rais,lakini akawashtumu watu ambao hakuwataja kwa kuleta migawanyiko kwa manufaa yao ya kibinafsi.

Also Read
Ruto Azungumza Kwa Mara Ya Kwanza Baada Ya Safari Yake Ya Uganda Kutibuka

Baadhi ya mawaziri na maafisa wa chama cha Jubilee hivi majuzi walimshtumu naibu rais William Ruto kwa kumhujumu rais huku wakimtaka kujiuzulu serikalini.

Also Read
Mbogo Awatahadharisha Wakaazi Wa Mombasa Dhidi Yakuchagua Viongozi Wasiokua Na Mwelekeo

Wakati huo huo, Ruto  aliunga mkonono hatua ya baadhi ya makanisa ya kupiga marufuku siasa kanisani.

Kanisa katoliki na lile la Kianglikana yalipiga marufuku siasa kwenye makanisa hayo yakisema wanasiasa wanahujumu maeneo ya sala.

Also Read
Naibu rais William Ruto asisitiza kuwa kukataliwa kwa BBI kulitarajiwa

Kauli yake inajiri baada ya kongamano la maaskofu wa kanisa katoliki nchini kutoa wito wa maridhiano kwa wawili hao kwa umoja wa taifa hili wakisema kuwa wako tayari kuongoza maridhiano hayo iwapo watahusishwa.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi