Nakubali Chaguo Lenu Asema Shaban

Mbunge wa Taveta Naomi Shaban amekubali  kushindwa kwenye kinyanyang’anyiro cha kuhifadhi kiti chake baada ya kuhudumu bungeni kwa miaka 20.

Mapema siku ya Jumatano alikubali kushindwa kupitia ujumbe wa Whatsapp huku akisema kwamba watu wa Taita Taveta wangependa kiongozi mpya na hata kumupongeza mpinzani wake John Bwire Okano mgombea wa chama cha Wiper.

Also Read
Msihusishe ugonjwa wa kifafa na ushirikina asema Daktari Chengo.

Alitoa tangazo hili baada ya matangazo ya awali kubaini kwamba Okano alikuwa anaongoza na wingi wa kura.

Okana ni wakili anayetoka hapa Mombasa aliyejitosa kwenye uchaguzi kwa mara ya kwanza.

Shaban mwenye umri wa miaka 58 alikuwa anatetea kiti chake kupitia tikiti ya chama cha Jubilee.

Also Read
Usalama waimarishwa Taita Taveta

Alingia mamlakani mwaka 2002 baada ya kuchaguliwa kwa tikiti ya chama cha KANU .

Mwaka 2007 alichaguliwa tena kwa tikiti ya chama cha KANU, na mwaka 2013 alitetea kiti chake kwa tikiti ya TNA . Na alichaguliwa tena mwaka 2017 licha ya kuwepo ya madai ya dosari ya uchaguzi kutoka kwa mpinzani wake Morris Mutiso

Also Read
Mitihani ya kitaifa yaendelea bila visa vya udanganyifu Taita Taveta

Kwenye serikali ya rais Kibaki alihudumu kama waziri wa mipango maalum kati ya mwaka 2008 na 2010 na kisha kuhamishwa hadi afisi ya jinsia na mwasala ya watoto.

 

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi