Ndege yaanguka barabarani na kuuwa watu sita

Ndege ndogo imeanguka kwenye barabara kuu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince na kusababisha vifo vya takriban watu sita.

Ndege hiyo ilikuwa njiani kutoka mji mkuu kuelekea mji wa bandari wa kusini-mashariki wa Jacmel ilipoanguka katika kitongoji cha Carrefour.

Also Read
Mwanaume Australia ashtakiwa kwa kumteka nyara mtoto wa miaka minne

Rubani alikuwa mmoja wa wale ambao awali walinusurika lakini alikufa kutokana na majeraha yake hospitalini baadaye.

Maafisa walisema kufeli kwa injini ndio tatizo. Ndege hiyo ilikuwa imetuma ishara ya itilafu dakika 20 baada ya kupaa, mamlaka ya usafiri wa anga nchini ilisema.

Also Read
Vitambulisho 700 Vya Kitaifa Havijachukuliwa Lamu

Waziri Mkuu Ariel Henry alituma risala zake za rambi rambi kwa familia za wahanga.

Nchi hiyo masikini imekumbwa na majanga kadhaa ya asili katika miaka ya hivi karibuni ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na uchumi.

Also Read
VVD Yashinda Uholanzi

Vurugu za magenge pia zimezidi kuwa mbaya kutokana na mzozo wa kisiasa kufuatia mauaji ya Rais Jovenel Moïse Julai mwaka jana.

  

Latest posts

Ujenzi Wa Nyumba Za Gharama Nafuu Wafaa Kufanywa Nje Ya Jiji Asema Thoya

Clavery Khonde

Tedros Adhanom Ghebreyesus Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu Wa WHO

Clavery Khonde

Jurgen Klopp Achaguliwa Kama Mkufunzi Bora Wa Ligi Ya EPL

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi