Naibu wa rais Dkt Willam Ruto anatarajiwa kuzuru eneo la Pwani kuanzia leo ili kujitafutia uungwaji mkono katika azma yake ya kuwania kiti cha urais mwaka ujao.
Ruto anatarajiwa kuzuru kaunti za Taita-Taveta na Kwale hii leo kujipigia debe katika safari yake ya kuelekea ikulu mwakani.
Akithibitisha hayo mbunge wa Msambweni Feisal Bader amesema Ruto atakuwa eneo bunge la Matuga kwa hafla ya miradi ya maendeleo inayowalenga vijana wa bodaboda na wafanyibiashara wadogo wadogo.
Amedokeza kwamba naibu rais atakuwa Ukunda siku ya Ijumaa kwa hafla ya kuchangisha fedha za kuwasaidia vijana wa bodaboda na wafanyibiashara.
Naibu huyo wa rais anatarajiwa pia kuzuru kaunti za Kilifi, Mombasa na Lamu kuwarai wakaazi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili wa wapiga kura wapya.