Mshirikishi wa muungano wa Kenya kwanza kaunti ya Kwale Mshenga Vuyaa Ruga ameipongeza hatua ya chama cha PAA ya kujiunga na muungano huo.
Kulingana na Ruga hatua hiyo itaimarisha muungano huo katika eneo la Pwani ili kuhakikisha unajizolea kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Akizungumza eneo la Ukunda Ruga amesema kuwa sasa muungano huo unaoungwa mkono na gavana wa Kwale Salim Mvurya na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi utakuwa na nguvu Pwani.
Wakati uo huo amebainisha kuwa umaarufu wa chama cha ODM umefifia ikilinganishwa na chama cha UDA katika kaunti ya Kwale.
Haya yanajiri wakati ambapo kinara wa ODM Raila Odinga anafanya ziara yake kaunti hiyo kupigia debe azma yake ya urais kupitia muungano wa Azimio-One Kenya.