Maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi yanapoendelea kuongezeka, baadhi ya wakaazi wa eneo hili wameibua hisia mseto kufuatia hatua ya watu kutotilia maanani masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.
Wakiongozwa na Robert Omari mkaazi wa Malindi ametaja hatua ya watu kupuuza masharti hayo ikiwemo kuvalia barakoa na hata kukaa umbali wa mita moja unusu huku akitaja baadhi ya hoteli kutokuwa na sabuni ama hata vieyuzi vya kutakasia mikono kabla ya wateja kuingia hali ambayo anasema inatahatarisha maisha ya watu.
Hata hivyo kwa upande wake Eddie Kahindi amewalaumu maafisa wa usalama kwa kuitisha hongo wanapowapata watu hawajavalia Barakoa na kukitaja kitendo hicho kama kinachowafanya wenyeji kuwa na dhana ya kutokuwepo na ugonjwa wa Covid-19 .