Raia wa Rwanda aregeshwa nchini humo kutoka Uswidi kujibu tuhuma za mauaji ya kimbari

Mamlaka ya Uswidi imemrejesha Mnyarwanda Jean Paul Micomyiza mjini Kigali kwa tuhuma za mauaji ya kimbari anayotuhumiwa kuyatekeleza alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Upande wa mashtaka wa Rwanda ulisema ulimpokea Jean siku ya Jumatano na kuipongeza Sweden kwa mchango wake “kupambana na kutokujali”.

Micomyiza mwenye umri wa miaka 50 alikamatwa nchini Uswidi mnamo Novemba mwaka 2020 baada ya Ruwanda kutoa hati ya kukamatwa kwake.

Ameishi Sweden kwa zaidi ya muongo mmoja. Anatuhumiwa kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa kujitwika jukumu la kuwasaka na kuwatambua Watutsi ili wauawe wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, alipokuwa na umri wa miaka 22.

Wakati huo, alikuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda kilichoko katika mji aliozaliwa, Butare, kusini mwa Rwanda.

Bw Micomyiza hajazungumza lolote kuhusu mashtaka anayokabiliwa nayo nchini Rwanda.

Alipoteza rufaa dhidi ya kurejeshwa kwake Desemba mwaka jana.

  

Latest posts

Tedros Adhanom Ghebreyesus Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu Wa WHO

Clavery Khonde

Koome Awapa Ilani Mawakili

Clavery Khonde

Wanasiasa Wahimizwa Kuhubiri Amani

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi