Raila Amteua Martha Karua Kama Mgombea Mwenza Wake

Martha Karua ndie mgombea mwenza wa mgombea wa urais kupitia chapa cha azimio la umoja one Kenya Raila Odinga.

Akitoa tangazo hilo katika jumba la mikutano ya kimataifa Raila Odinga amemtaja Karua kama kiongozi shupavu ambaye hayumbishwi na mawimbi ya kisiasa.

Amesema Karua ni mwanamke ambaye amepigania mageuzi kwa muda mrefu na anauwezo mkubwa wakuliboresha taifa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Also Read
Jamii Ya Wamakonde Yawataka Wanasiasa Kutowashurutisha Kuwapigia Kura

Wakati huo huo Odinga amemteua Karua kama waziri wa wizara ya sheria na katiba endapo atachaguliwa kama rais wa tano wa jamhuri ya Kenya.

Also Read
Raila ajitenga na madai kuwa alisababisha serikali ya Jubilee kutotekeleza miradi yake ipasavyo

Baada ya kuteuliwa kama mgombea mwenza Martha Karua amesema hii ni safari ya wakenya wote huku akisema yuko tayari kwa kibarua hicho kipya kama wakenya watamuidhinisha Raila kama rais.

Amewahakikishia wakenya kuwa atahakikisha swala la ufisadi linatokomezwa.

Wakati huo huo Raila Odinga amewateua Hassan Joho kama waziri wa kilimo, Wyclif Oparanya akipendekezewa wizara ya fedha huku Peter Munya akipendekezwa kuwa waziri wa kilimo na kinara wa chama cha Wyper Kalonzo Msyoka akipendekezewa waziri mkuu naye Kenneth Marende akipendekezewa kuwa spika wa bunge la seneti.

  

Latest posts

Ofisi Ya Msajili Yawashirikisha Washikadau Kwenye Msafara Wa Amani Pwani

Ruth Masita

Nzai Aeleza Nia Ya Kuimarisha Viwango Vya Elimu Jomvu

Ruth Masita

WRC Safari Rally Kuandaliwa Naivasha

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi