Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ametangaza rasmi kuwa yupo tayari kuliongoza taifa hili endapo wakenya watampa fursa ya kufanya hivyo.
Akihutubu katika kongamano la Azimio la umoja lilowaleta pamoja viongozi mbali mbali kutoka vyama tofauti humu nchini, kinara huyo ameweka wazi kuwa atakua kwenye kinyng’anyiro cha mwaka 2022.
Aidha amesema nchi hii inahitaji kuwa na umoja zaidi huku akiwataka wakenya kuzidi kuishi kwa utangamano.
Raila amesema yeye maazimio yake makuu si kushindana bali ni kubadilisha uchumi wa nchi kwa mawazo ambayo yataleta mafanikio kwa taifa hili.
Aidha ametangaza kubuniwa kwa vuguvugu la Azimio la umoja movement ambalo litawajumuisha wakenya wote.
Odinga ameendelea kusifia maridhiano aliyoyafanya na rais Uhuru Kenyatta akisema maridhiano hayo yameweza kuleta umoja zaidi na amani nchini.