Mgombea urais kupitia muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga ameanza rasmi ziara yake katika ukanda wa pwani.
Akizungumza katika kaunti ya Tana River odinga amesema kuwa nia yake kubwa ni kuboresha maisha ya wakenya wa chini kwa kuhakikisha kuwa jamii inawezeshwa kuwa na afya bora.
Wakati huo huo ameendelea kupigia debe mpango wa kuzipatia familia maskini shilingi elfu sita kila mwezi huku pia akisema anachotaka kukileta ni mapinduzi ya uchumi.